News Details

Event

Mzumbe Wanyakua Ushindi Mnono Maonesho Ya Biashara Kimataifa [Sabasaba]

16 Jul Joseph Kiphizi Sat 16 Jul 2022

Chuo Kikuu Mzumbe kimeibuka mshindi wa nafasi ya pili kwa Taasisi za Elimu ya juu kipengele cha Utafiti na Uendelezaji wa bunifu katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yaliyohitimishwa Julai 13 mwaka huu

Akizungumza na Washiriki waliokiwakilisha Chuo katika maonesho hayo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka, amewashukuru na kuipongeza timu hiyo ya Wanajumuiya ya Chuo Kikuu Mzumbe, walioshiriki kwa namna mbalimbali katika maonesho hayo, na kuongeza kuwa ushindi huo umepatikana kutokana na uwekezaji wa jitihada na bidii kubwa.

“Nimepokea ushindi huu kwa heshima kubwa sana ,hakika ninajivunia mno ushindi huu ambao umekuja baada ya kazi kubwa mliyoifanya,nawapongeza sana timu pamoja na wote walioshiriki kuandaa”.Alisema

Kwa upande wao Washiriki waliokiwakilisha chuo, wameshukuru Menejimenti ya chuo kwa kuwaamini ,kuwapatia nafasi hiyo adhimu ya uwakilishi pamoja na ushirikiano wa bega kwa bega uliopelekea kuleta mafanikio ya ushindi huo na kuahidi kkuongeza juhudi  na maarifa katika maonesho yajayo.

Chuo kikuu Mzumbe kimeshika nafasi ya Pili, nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Taasisi ya Uhasibu Arusha, na Nafasi ya Tatu kunyakuliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  Maonesho ya 46 ya kibiashara ya kimataifa yamehitimishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Phillip Mpango.

Kwa habari zaidi na picha,Bofya haya

0 Comments

No Comments at the moment