News Details

Event

Siku Ya Mzumbe Na Kambi Ya Ujasiriamali (Simkau) : Rc Morogoro Awaanza Mzumbe Kujikita Kwenye Ujasiliamali

12 May Joseph Kiphizi Thu 12 May 2022

Mkuu wa mkoa Morogoro Martine Shigela amewataka wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe pamoja na vyuo vingine mkoani humo kujikita katika ujasiriamali pindi wawapo chuoni ili kujiingizia kipato

RC Shigella ametoa wito huo wakati akifungua kongamano la ujasirimali lilofanyika chuo kikuu Mzumbe ambalo linafahamika kama Mzumbe day ambapo amesema wapo baadhi ya wanafunzi wana mawazo ya kizamani ya kutegemea mikopo pekee badala ya kufanya shughuli zingine.

"Sisi wakati tunasoma tukimaliza tunapangiwa ajira siku hiyo hiyo unachagua mwemywe lakini kwa sasa idadi ya wasomi imeongezeka hivyo ajira za serikali ni chache lazima wanafunzi wajiongeze "

Katika hatua nyingine Rc Shigella amekipongeza chuo cha Mzumbe kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya ujasirimali jambo ambalo linazalisha wasomi wenye weredi na maarifa makubwa katika utendaji kazi.

Shigela amevitaka vyuo vingine binafsi na Serikali Mkoani humo kuiga mfano huo kwani unaondoa malalamiko ya ajira kwa Serikali.

Awali ,Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lugano kusiluka amesema progamu hiyo imeanza mwaka 2017 na inafanyika kila mwaka huku lengo likiwa kuongeza hamasa kwa wanafunzi kuwa na moyo wa kujiajiri badala ya kusubiri ajira za serikali

0 Comments

No Comments at the moment