News Details

Event

Tanzia: Kifo Cha Ismail A. Ismail Aliyekuwa Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Mzumbe

04 Dec Joseph Kiphizi Mon 04 Dec 2023

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mwanafunzi na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe(MUSO) mwaka 2022/2023, Bwn Ismail A. Ismail.

Bwn.  Ismail amehitimu Shahada ya Utawala wa Umma(BPA) aliyotunukiwa katika mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe 23/11/2023.

Kifo hicho kimetokea 1 Disemba 2023 kwa ajali ya gari. Mazishi yamefanyika 2 Disema 2023 katika eneo la Itaga (makaburi ya familia).

Chuo Kikuu Mzumbe kinatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

1 Comments

Kyejoaugustino22@Gmail.Com - Wed 07 Feb 2024 13:48 p.m.
REST IN ETERNAL WAZIRI MKUU WETU