News Details

Event

Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe Wajitokeza Kuchangia Ujenzi Wa Hosteli Maonesho Ya Sabasaba

04 Jul Joseph Kiphizi Tue 04 Jul 2023

Wananchi mbalimbali wakiwemo Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe wameendelea kutembelea katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara la Kilwa jijini Dar es Salaam Dar es Salaam ili kujifunza na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.
Baadhi ya Wahitimu waliofika kwenye banda hilo wameguswa na kampeni ya Harambee ya Ujenzi wa Hostel ya wanafunzi wa kike katika Ndaki ya Mbeya na wao kuamua kuchangia papo hapo na kuendelea kuwahamasisha Watanzania na wahitimu wengine kushiriki katika harambee hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Homera ambayo imelenga kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu nchini
Bw. Amon Msonga Mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe mwaka 2022 kwa Shahada ya Umahiri katika Masoko, ameomba wahitimu wote waliomaliza Chuo Kikuu Mzumbe kujitokeza ili kushirikiana na Chuo kufanikisha ujenzi wa hosteli hiyo Ndaki ya Mbeya kwa ustawi wa Elimu nchini.
"Nipende kutoa wito kwa Watanzania na Wahitimu wenzangu wa chuo Kikuu Mzumbe wa kampasi zote kujitokeza kuunga mkono harambee ya kuchangia ujenzi wa hostel kwani hatua za uchangiaji ni rahisi sana kupitia (Control number 994180331310) ambapo unaweza kuchangia ukiwa popote na kiasi chochote cha fedha kwa kutumia mitandao yote ya simu nchini na benki yeyote na fedha hiyo itaingia katika akaunti ya chuo moja kwa moja na hivyo utakuwa umechangia ujenzi huo na kuwa sehemu ya historia ya ujenzi huo na Mzalendo kwa Taifa lako”Alisisitiza Msonga
Kwa Upande wake Martine Thomas Mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe mwaka 2021 kwa Shahada ya Umahiri katika Masoko, amesema wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa umoja wao wanao uwezo wa kukiwezesha chuo kufikia malengo yake kwa kuchangia ujenzi wa hosteli hiyo kwani itasaidia wadogo zao kukaa mahali salama na kuwasisitiza Wahitimu wenzake kuitikia wito wa kuchangia ujenzi huo.
“Kaulimbiu ya Chuo Chetu ni Tujifunze kwa maendeleo ya watu, nawasihi wahitimu wenzagu tuunge mkono jitihada za chuo kwa kuchangia kiasi chochote kwani hosteli hiyo itasaidia wadogo zetu na hata watoto wetu hapo baadaye”. Alisisitiza Bw. Thomas.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Ukimataifishaji na Baraza la Wahitimu Dkt. Lucy Massoi amewashukuru wale wote waliotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe na kuchangia ujenzi huo na amewaomba Watanzania wote kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia ujenzi wa hosteli hiyo Kupitia namba ya malipo (control number)994180331310

 

Kwa picha zaidi za matukio yanayoendelea kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe,Bofya hapa kutembelea ukurasa wetu wa Facebook

0 Comments

No Comments at the moment